NyumbaniHome / HabariNews

Habari na MatukioNews & Events

Yanayoendelea Vivid Dream SchoolsWhat's happening at Vivid Dream Schools

Matangazo kwa wazazi, ofa, mahafali na matukio ya shule, yote mahali pamoja.

Notices for parents, offers, graduations and school events, all in one place.

Kwa Wazazi · Sasa HiviFor Parents · Right Now

Matangazo muhimuImportant notices

10–20 Novemba 202610–20 November 2026

Thibitisha nafasi ya mtoto wako kwa mwaka 2027Confirm your child's place for 2027

Wazazi wa Baby class hadi Darasa la Saba: lipa TSh 200,000 kati ya tarehe 10 na 20 Novemba 2026 kuthibitisha kuwa mtoto ataendelea na masomo mwaka 2027. Si malipo ya ziada, ni sehemu ya awamu ya kwanza; salio la awamu ya kwanza ni TSh 185,000.

Parents of Baby class to Standard 7: pay TSh 200,000 between 10 and 20 November 2026 to confirm your child continues in 2027. It is not an extra charge, it is part of the first instalment; the balance of the first instalment is TSh 185,000.

Ada 20272027 fees

Hadi 11 Januari 2027Until 11 January 2027

Ofa maalum ya ada 2027, okoa TSh 70,000Special fee offer 2027, save TSh 70,000

Lipa ada na chakula ya mwaka mzima (kawaida TSh 1,225,000) kwa mara moja kabla ya 11 Januari 2027 ulipe TSh 1,155,000 tu, punguzo la 5.7%. Kamilisha malipo, imarisha maendeleo.

Pay the full year of tuition and meals (normally TSh 1,225,000) in one payment before 11 January 2027 and pay only TSh 1,155,000, a 5.7% discount. Complete your payment, strengthen progress.

Tazama tangazoView the poster

Desemba 2026December 2026

Programu maalum ya Qur'an, DesembaSpecial December Qur'an programme

Likizo yenye baraka: Qur'an Tahfidh (kuhifadhi) TSh 100,000 kwa mwezi, na Qur'an Tilawa (kusoma kwa usahihi) TSh 70,000 kwa mwezi. Ni hiari; fika shuleni kuchukua na kujaza fomu. Chakula kinatolewa; usafiri ni wa mzazi.

A blessed holiday: Qur'an Tahfidh (memorisation) TSh 100,000 a month, and Qur'an Tilawa (correct recitation) TSh 70,000 a month. Optional; collect and fill in the form at the school. Meals are provided; transport is by parents.

Maelezo kamiliFull details

20 Novemba 202620 November 2026

Shule inafungwa 20 Novemba 2026School closes on 20 November 2026

Baada ya Darasa la Saba kumaliza mitihani ya taifa salama, masomo ya Madrasa yanaendelea hadi shule itakapofungwa tarehe 20 Novemba 2026, Insha'Allah.

After Standard 7 have safely completed their national exams, Madrasa lessons continue until school closes on 20 November 2026, Insha'Allah.

Kidato cha Kwanza 2027Form One 2027

Kutoka Vivid Dream Primary kwenda SekondariFrom Vivid Dream Primary to Secondary

Mahitaji ya kujiunga: fomu maalum ya kujiunga, sare za shule (jozi 2) TSh 100,000, sare za dakhalia na jezi ya michezo TSh 200,000, kitanda TSh 100,000 na tablet ya masomo TSh 350,000, jumla TSh 750,000, yanalipwa ofisini.

Joining requirements: a joining form, school uniform (2 sets) TSh 100,000, boarding uniform and tracksuit TSh 200,000, bed TSh 100,000 and a study tablet TSh 350,000, total TSh 750,000, paid at the school office.

Ada ya SekondariSecondary fees

Udahili unaendeleaAdmissions open

Kidato cha Tano, Vivid Dream High SchoolForm Five, Vivid Dream High School

Tahasusi za sayansi, biashara na sanaa, dakhalia bure kwa wanafunzi wote na milo mitatu kwa siku.

Science, business and arts combinations, free boarding for all students and three meals a day.

Tahasusi na adaCombinations & fees

App ya Wazazi · BureParent App · Free

Matokeo na malipo ya mwanao, kwenye simu yakoYour child’s results and payments, on your phone

Tafuta: Inspire School (Parent), app yenye rangi ya kahawaSearch for: Inspire School (Parent), the brown app

  1. 1Futa app yoyote ya zamani ya Inspire, kisha pakua Inspire School (Parent).Delete any old Inspire app, then download Inspire School (Parent).
  2. 2Bonyeza SELECT SCHOOL, shuka mwisho wa orodha, chagua Vivid Dream Primary School au Vivid Dream Secondary School, kisha Submit.Tap SELECT SCHOOL, scroll to the end of the list, pick Vivid Dream Primary School or Vivid Dream Secondary School, then Submit.
  3. 3Ingia: namba yako ya simu (Primary anza na 0, Secondary anza na +255); nenosiri ni tarakimu 6 za mwisho za namba hiyo.Log in: your phone number (Primary starts with 0, Secondary with +255); the password is its last 6 digits.

Maelekezo kamili na videoFull guide with video

Walimu na wafanyakazi: tumieni app ya Inspire School (Staff), Teachers and staff: use the Inspire School (Staff) app, iPhone · Android · portal ya walimustaff portal: MsingiPrimary / SekondariSecondary

8 Novemba 2026 · Ukumbi wa SUZA8 November 2026 · SUZA Hall

Mahafali ya Tano5th Graduation

KG2 na Kidato cha Nne, Class of 2026KG2 and Form Four, Class of 2026

Vivid Dream Schools ilifanya mahafali yake ya tano katika Ukumbi wa SUZA, Zanzibar, kwa wahitimu wa KG2 na Kidato cha Nne, Class of 2026. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mboja Ramadhan Mshenga, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (SMZ). Hafla ilihusisha utoaji wa vyeti, tuzo na heshima, hotuba za mafanikio na sherehe ya maendeleo ya watoto wetu.

Vivid Dream Schools held its fifth graduation at SUZA Hall, Zanzibar, for KG2 and Form Four graduates, the Class of 2026. The guest of honour was Hon. Mboja Ramadhan Mshenga, Deputy Minister of Education and Vocational Training, SMZ. The day included certificates, awards and honours, speeches on achievement and a celebration of our children's progress.

Tazama videoWatch the videoPicha zaidiMore photos

Mgeni rasmi akihutubia Utoaji wa vyeti Wahitimu wa KG2 Wazazi na wageni

Kalenda ya MatukioEvents Timeline

Mwaka wa mafanikioA year of achievement

24 Novemba 202624 November 2026

App mpya ya wazazi: Inspire School (Parent)New parent app: Inspire School (Parent)

Wazazi sasa wanaona matokeo na taarifa za malipo ya mtoto kwenye simu, bure. Maelekezo ya hatua kwa hatua na video fupi yako kwenye ukurasa wa wazazi.Parents can now see their child’s results and payment details on the phone, free. A step-by-step guide and a short video are on the parents’ page. Jinsi ya kuanzaHow to start →

22 hadi 24 Novemba 202622 to 24 November 2026

Mafunzo ya mifumo ya TEHAMA (ICT) kwa walimu na wafanyakaziICT systems training for teachers and staff

Kwa siku tatu, walimu na wafanyakazi wa Vivid walijifunza kutumia mfumo wa kidijitali wa shule: mahudhurio, mitihani, scheme of work na lesson plan. Matokeo yake kwa mzazi: taarifa za mwanao zinafika haraka na kwa usahihi kwenye app ya wazazi.Over three days, Vivid teachers and staff learned to use the school’s digital system: attendance, examinations, schemes of work and lesson plans. What it means for parents: your child’s information reaches the parent app faster and more accurately. PichaPhotos →

8 Novemba 20268 November 2026

Mahafali ya Tano, KG2 na Kidato cha Nne5th Graduation, KG2 and Form Four

Ukumbi wa SUZA. Mgeni rasmi: Mh. Mboja Ramadhan Mshenga, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (SMZ).SUZA Hall. Guest of honour: Hon. Mboja Ramadhan Mshenga, Deputy Minister of Education and Vocational Training, SMZ. VideoVideo →

1–4 Novemba 20261–4 November 2026

Ugeni wa IHH Netherlands pamoja na NAYFIHH Netherlands visit with NAYF

Ugawaji wa cherehani kwa mafunzo ya ushonaji Mbuzini na programu ya chakula bure kwa wanafunzi.Sewing machines handed over for tailoring training at Mbuzini, and a free meal programme for students.

Oktoba, Novemba 2026October, November 2026

Mitihani ya taifa: Kidato cha Pili, Darasa la Saba na Kidato cha NneNational exams: Form Two, Standard 7 and Form Four

Tuliwaombea dua na kuwatakia kheri watahiniwa wetu wote; Darasa la Saba walimaliza salama na kurudi nyumbani salama.We prayed for and wished all our candidates well; Standard 7 finished safely and returned home safely.

24 Septemba 202624 September 2026

Mashindano ya sayansi, Chuo cha Ualimu Nkrumah: nafasi ya 3Science competition, Nkrumah Teachers' College: 3rd place

Vivid ilishika nafasi ya 3 kati ya shule 11 zilizoshiriki.Vivid came 3rd out of 11 participating schools.

18 Septemba 202618 September 2026

Young Scientists Tanzania: nafasi ya 19 kati ya shule 1,330Young Scientists Tanzania: 19th of 1,330 schools

Mradi wa wanafunzi wetu, "Assessment of Air Pollution and Its Impact on Rainwater Quality", uliingia shule 45 bora na kushika nafasi ya 19 kati ya shule 1,330.Our students' project, "Assessment of Air Pollution and Its Impact on Rainwater Quality", reached the top 45 and placed 19th out of 1,330 schools.

10 Agosti 202610 August 2026

Siku ya Vivid Dream SchoolVivid Dream School Day

Kutoka wanafunzi 300 na walimu 21 mwaka 2019, Vivid imekua hadi kuwa na maeneo Unguja na Pemba.From 300 students and 21 teachers in 2019, Vivid has grown into schools across Unguja and Pemba.

1 Agosti 20261 August 2026

Kongamano la Kwanza la Shule zenye Madrasa ZanzibarFirst Conference for Schools with Madrasas in Zanzibar

Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Mazizini, kwa kushirikiana na Noor Al Yaqeen Foundation. Mgeni rasmi: Naibu Mufti wa Zanzibar.Office of the Chief Mufti of Zanzibar, Mazizini, organised with the Noor Al Yaqeen Foundation. Guest of honour: the Deputy Mufti of Zanzibar.

20262026

Vivid Dream High School yaanza Kidato cha TanoVivid Dream High School opens Form Five

Tahasusi 8 za sayansi, biashara na sanaa katika jengo la Ummul Mu'minin Aisha, Kinduni, dakhalia bure kwa wote.Eight science, business and arts combinations in the Ummul Mu'minin Aisha building, Kinduni, free boarding for all.

28 Machi 202628 March 2026

Siku ya Kifaransa (Francophonie)Francophonie Day

Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu aliwasilisha hotuba kwa Kifaransa; shule ilipata cheti cha ushiriki.A Form Three student gave a speech in French; the school received a certificate of participation.

7 Februari 20267 February 2026

Dua ya Shukrani: matokeo ya kwanza ya Kidato cha NneThanksgiving dua: our first Form Four results

Wanafunzi wote 25 walifaulu (GPA 2.4360, NECTA), na wanafunzi 6 waliopata Daraja la Kwanza walialikwa kwenye hafla ya kupongezwa na Rais wa Zanzibar.All 25 candidates passed (GPA 2.4360, NECTA), and the 6 Division One students were invited to a congratulation event with the President of Zanzibar.

13 Desemba 202513 December 2025

Mahafali ya kwanza ya Kidato cha NneFirst Form Four graduation

Chuo cha Ualimu Nkrumah. Tuzo za "Outstanding Performance Award 2025" zilitolewa kwa msaada wa Noor Al Yaqeen Foundation.Nkrumah Teachers' College. "Outstanding Performance Award 2025" awards were presented with support from the Noor Al Yaqeen Foundation. VideoVideo →

6 Desemba 20256 December 2025

Matokeo ya Darasa la Saba 2025: ufaulu 100%Standard 7 results 2025: 100% pass rate

Wanafunzi wote 98 wamefaulu (BMZ).All 98 candidates passed (BMZ). MatokeoResults →

22 Novemba 202522 November 2025

Mahafali ya KG2, MbuziniKG2 graduation, Mbuzini

Watoto wetu wa KG2 walihitimu elimu ya maandalizi mbele ya wazazi na walimu.Our KG2 children graduated from nursery in front of parents and teachers. VideoVideo →

12 Septemba 202512 September 2025

Dua kwa wanafunzi wa Kidato cha PiliDua for our Form Two students

Shughuli ya dua ya pamoja kuwaombea wanafunzi wa Kidato cha Pili kuelekea mitihani ya taifa.A shared dua gathering for our Form Two students ahead of their national exams.